CHF Iliyoboreshwa

Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Ilianzishwa) na Serikali  kwa  sheria  ya mwaka 2001; ambapo kila  Halmashauri ilitakiwa kuanzisha Mfuko  wa CHF. Tathmini ya uendeshaji wa mfuko huu imeonesha  kwamba utekelezaji wake unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatokana  na  matatizo  ya  muundo na  mfumo  wa  uendeshaji wake;  matokeo yake  kumekuwa na  mafanikio  tofauti baina   ya  Halmashauri moja na nyingine.

Kufuatia  changamoto  hizo   Serikali   imedhamiria kufanya maboresho katika maeneo matatu ili kuimarisha uendeshaji wa  Mfuko wa Afya ya Jamii.Maeneo hayo ni;Usimamizi na Uendeshaji (Governance),Usajili wa wanachama wa Mfuko   (Enrolment),  Kitita cha mafao na ngazi ya upatikanaji wa huduma za Afya (Benefit Package).

Soma zaidi

Kitita cha mafao ya CHF

Mwanachama wa CHF atapata huduma zote za matibabu kwa kufuata utaratibu wa rufaa kwa ngazi zote za vituo vya kutolea huduma vya serikali.

Utaratibu wa Kuandikishwa/Kuhuishwa

Kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii ( CHF Iliyoboreshwa) tembelea Ofisi ya Mtaa / Kijiji kwa Afisa Mwandikishaji au kwa wakala aliye idhinishwa, utafamyiwa usajili wa kaya kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ya simu ya mkononi.  Ambapo kila mwanachama atapigwa picha bure na kupewa kitambulisho.

Pia kwa mwanachama aliyefikia kikomo cha Uanachama wake utahuishwa kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ya simu ya mkononi.

Habari za CHF Habari zaidi

Jul
21
CHF ILIYOBORESHWA MKOMBOZI WA WATANZANIA
Sekta ya Afya nchini Tanzania katika kipindi hiki cha miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano, ime...

Jul
21
WANANCHI WAFAIDIKA NA BIMA YA CHF ILIYOBORESHWA
Sekta ya Afya nchini Tanzania imezidi kupiga hatua katika kuboresha huduma. Wananchi wameendelea kuf...

Jul
21
CHF ILIYOBORESHWA YAFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA
Kulingana na tafiti zisizo rasmi inaonyesha kuwa watu wengi wana uelewa kuhusiana na CHF ya zamani a...