.

CHF in News

WANANCHI WAMSHUKURU DIWANI WAO KWA KUWAKATIA BIMA ZA AFYA 144
Posted on Apr 20, 2021

Wananchi wa Kata ya Majengo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamemshukuru Diwani wao Mhe.William Mbogo kwa kuwakatia Bima za Afya CHF iliyoboreshwa baadhi ya Wakazi wa Kata yake wanaoishi katika mazingira magumu ambapo Kaya 24 zenye wanufaika 144 zimesaidiwa. Kadi hizo za Bima ya Afya iliyoboreshwa kwa wakazi wa Kata ya Majengo,zimekabidhiwa mbele ya Mgeni rasmi katika tukio hilo ambae ni pia Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Kimaro akiongozana na Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda,Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya limefanyika katika Kituo cha Afya Town Clinic kilichopo Manispaa ya Mpanda.
Akikabidhi Kadi hizo za Bima ya Afya iliyoboreshwa Diwani wa Kata ya Majengo William Mbogo amesema amefanya hivyo baada ya kuona umuhimu wa afya kwa wananchi wake hivyo kuanzisha kwake kutawafanya wananchi kuona umuhimu wa kuwa na Bima za Afya.